Katika shamrashamra za maonesho ya wakulima Nanenane 2025, zaidi ya wananchi 300 wamejitokeza kwa wingi kujionea ubunifu na mafanikio ya sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na bidhaa za usindikaji kutoka kwa wajasiriamali wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Miongoni mwa vivutio vikuu kwenye maonesho hayo ni zao la Muhogo aina ya Kiroba na Chereko lililowasisimua wengi katika Banda la Wilaya ya Nyasa.
Theresia Paulo Ndunguru, mkulima shupavu kutoka Kijiji cha Ngindo, Wilaya ya Nyasa, amewapa elimu ya kina wananchi kuhusu manufaa makubwa ya zao hilo linalolimwa kandokando ya Ziwa Nyasa.
“Muhogo si chakula tu – ni mali!”
Akitaja matumizi yake:
Ugali
Biskuti
Tambi
Keki
Mkate
Magadi & Chumvi ya Asili
Amesisitiza kuwa Muhogo unalima kwa gharama ndogo na hulipa kwa faida kubwa, huku akihamasisha wananchi kwa msemo wake maarufu:
“Lima kwa tija, Muhogo unalipa!”
Jonas Mfunda (Rungwe), Thadeo Maulid (Songwe) na Nicholaus Mwamwaja (Mbeya) ni miongoni mwa waliovutiwa na elimu hiyo, wakiapa kuanza kilimo cha muhogo kwa majaribio kwenye maeneo yao.
Maonesho haya yanazidi kushika kasi!
Yamekusanya nguvu za mikoa minne: Ruvuma, Njombe, Iringa na Mbeya, yakiongozwa na kauli mbiu:
“Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”
Maonesho yataendelea hadi tarehe 8 Agosti!
#Nanenane2025 #KilimoBora #MuhogoUnalipa #BandaLaNyasa #MaendeleoVijijini #JohnMwakangaleGrounds #NyandaZaJuuKusini
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.