Halmashauri ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma imeanza rasmi ukarabati wa Stendi ya Mabasi ya Madaba.
Kazi ya awali inahusisha usawazishaji wa eneo la ndani la stendi, ikiwa ni mwanzo wa maboresho makubwa yanayolenga kuboresha huduma kwa abiria na kuchochea maendeleo ya usafiri wa umma katika eneo hilo.
Wananchi wa Madaba wamesema wanaupokea mradi huu kwa matumaini makubwa, wakiamini kuwa stendi hiyo mpya itarahisisha usafiri, kuongeza shughuli za kiuchumi, na kubadili kabisa sura ya mji wa Madaba kuwa kitovu cha biashara na huduma bora kwa wasafiri.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.