Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw. Eliud Sanga, akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene C. Isaka, wamemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, katika ofisi yake mjini Songea.
Katika mazungumzo yao, Bw. Sanga ameeleza kuwa ziara yao imelenga kuzungumza na watumishi wa NHIF pamoja na wadau. Pia kwa Mkoa wa Ruvuma ziara hiyo imelenga kukagua eneo wanalotarajia kujenga ofisi ya NHIF katika Manispaa ya Songea, ambapo ujenzi huo unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha ujao wa 2025/2026.
Kwa upande wake, Kanali Ahmed amesema Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya afya, hivyo amewasisitiza ofisi itakayojengwa inapaswa kuwa si tu ya kuvutia kimwonekano, bali pia iwe na uwezo wa kutoa huduma stahiki kwa wananchi na kuwafikia watu wengi.
Amebainisha kuwa wakazi wengi wa Mkoa wa Ruvuma ni wakulima wanaotegemea huduma bora za bima ya afya ili waweze kupata matibabu kwa wakati na kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji, hali itakayosaidia kuinua pato la mkoa na taifa kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.