• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yatekeleza ahadi sekondari ya wasichana Masonya

Imewekwa kuanzia tarehe: July 24th, 2025

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Masonya wilayani Tunduru wamefurahia kuanza kwa ujenzi wa bwalo la chakula, hatua ambayo inaondoa rasmi adha ya kula chakula chini ya miti au ndani ya madarasa. 

Furaha yao imeelekezwa kwa Serikali ya awamu ya sita, wakisema kuwa jitihada hizi zinaongeza thamani ya elimu na hadhi ya shule hiyo ya wasichana pekee katika wilaya.


Mwanafunzi Marian Michael, akizungumza kwa niaba ya wenzake, amesema kuwa bwalo hilo ni mkombozi mkubwa hasa ikizingatiwa ongezeko la wanafunzi wa kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2025/2026. 

Ameomba mradi huo ukamilishwe kwa wakati ili kutoa huduma mapema. 

Mkuu  wa shule hiyo, Makrina Ngonyani, amesema ujenzi ulianza Juni kwa kusafisha eneo na tayari kifusi kimeshajazwa katika msingi, huku hatua ya kumwaga zege ikisubiriwa.


Mradi huo unagharimu zaidi ya Shilingi milioni 168 ambapo hadi sasa zaidi ya milioni 102.7 zimetumika. 

Ameeleza kuwa shule hiyo imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitatu kupitia miradi ya ujenzi wa mabweni manne, madarasa, na vyoo kwa zaidi ya Shilingi milioni 775.


Katika ziara yake shuleni hapo, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,Mheshimiwa Denis Masanja, aliwataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili bwalo likamilike kabla ya msimu wa mvua. Amewapongeza walimu kwa usimamizi makini wa miradi, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwa na bidii, nidhamu na upendo kwa wanafunzi huku Serikali ikiendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi yao.


Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MARAIS watatu walivyoiandika historia katika kambi ya Muhukuru Songea

    July 25, 2025
  • MAMA auwa watoto watatu kwa kuwchinja Ruvuma

    July 25, 2025
  • RUVUMA kuandika historia mpya

    July 25, 2025
  • RAIS SAMIA kuzindua mradi wa uchimbaji Urani Namtumbo

    July 24, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.