Wakazi wa Mji wa Tunduru mkoani Ruvuma wana kila sababu ya kutabasamu baada ya Serikali ya awamu ya sita kutoa zaidi ya shilingi bilioni 3.4 kwa ajili ya kutatua tatizo sugu la uhaba wa maji safi na salama.
Fedha hizo zinakwenda kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya maji, na hatimaye kumaliza safari ndefu ya kina mama na watoto kutafuta maji kwa masafa marefu kila siku.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Tunduru, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tunduru Mjini (TUWASA),
Mhandisi Cuthbert Kiwia, alisema mradi huo mkubwa utaongeza uwezo wa uzalishaji maji hadi kufikia lita milioni 8.2 kwa siku. Hii ni zaidi ya mahitaji ya sasa ya mji huo ambayo ni lita milioni 6.8 kwa siku.
“Hii ina maana kuwa wakazi wa Tunduru sasa wataanza kupata huduma ya maji kwa asilimia 100,” alisisitiza Kiwia.
Mradi huo pia utahusisha ujenzi wa mtandao mpya wa mabomba wa kilomita 98.6, kutoka kilomita 3.3 za sasa. Zaidi ya hapo, tenki kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja linajengwa katika eneo la juu zaidi mjini humo, hatua itakayosaidia kusukuma maji hadi katika maeneo yaliyokuwa hayafikiki hapo awali.
Kwa mujibu wa Kiwia, mafanikio haya yametokana na juhudi za makusudi za Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Tangu aingie madarakani, miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4.8
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TUWASA, Jonathan Haule ametoa shukrani zake kwa Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi ili kuimarisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.