Asilimia 90 ya vitabu vya Tanzania havina maudhui ya ukweli kuhusu Uhuru wa Tanzania
Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema asilimia 90 ya vitabu vya Tanzania havina maudhui ya ukweli kuhusu Tanzania ilivyopata uhuru wake bila kumwaga damu .
Waziri Mwakwembe ameyasema hayo wakati alipotembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Mjini songea hivi karibuni katika ziara yake aliyoifanya mkoani Ruvuma ya kutembelea maeneo ya harakati za ukombozi dhidi ya wakoloni.
Amesema suala la kupata uhuru ni mchakato ,hivyo uhuru wa Tanzania haujapatikana kwa njia ambazo waandishi wa vitabu wamezitaja kwa sababu kuna wananchi walijitolea katika harakati za ukombozi hadi kumwaga damu.
Dkt.Mwakyembe akiwa katika Makumbusho ya Taifa ya Majimaji alishuhudia historia ya ukombozi iliyoanza wakati wa Vita vya Majimaji iliyofanyika mwaka 1905 hadi 1907 ambapo katika vita hivyo mashujaa 67 walivyongwa na kuzikwa kwenye makaburi yaliyopo ndani ya makumbusho hayo..
Kulingana na Mwakyembe,vitabu vingi vya Historia ya Upatikanaji wa Uhuru ya Tanzania inaonesha kuwa Tanzania bara ilipata Uhuru bila kumwaga damu jambo ambalo amesema sio sahihi kwa sababu tangu miaka ya Vita vya Majimaji Wananchi wa Tanganyika waliukataa Utawala wa Wajerumani ambao walikuwa wanaitawala Tanzania wakati ule ambapo baadhi yao walipoteza maisha kwa kumwaga damu.
“Mababu zetu walipigania uhuru kwa kumwaga damu kwa lengo la kupinga Utawala wa Wajerumani na ndipo walipoanzisha vita ya Majimaji na kupigana tangu mwaka 1905 hadi 1907 na ndipo mashujaa wa vita vya majimaji 67 walinyongwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja’’,alisisitiza.
Hata hivyo amesema vitabu vingi historia havionyeshi Tanzania ilipata Uhuru kwa Kumwaga damu,badala yake vitabu vinaonesha Tanzania ilipata Uhuru bila kumwaga Damu jambo ambalo Waziri Mwakyembe amesema hakubaliani na waandishi wa Historia ya Tanzania.
“Kwa kweli hapo sikubaliani na waandishi wa Historia ya Tanzania nafikiri waanzie mwanzo kabisa badala ya kuanzia wakati wa Uhuru’’,alisisitiza Dkt.Mwakyembe.
Dkt.Mwakyembe ameagiza kutunzwa kwa makaburi ya Mashujaa 67 waliozikwa katika Kaburi moja ndani ya Makumbusho ya Majimaji na kwamba mashujaa hayo walipinga Utawala wa Wajerumani.
Amesema wakoloni walikuwa wanyonyaji ambao waliwatumikisha wananchi kwa ujira mdogo na kulipa kodi kwa manufaa ya Utawala wa Ujerumani.
Waziri Mwakyembe ameshauri waandishi wa vitabu vya historia waanzie toka enzi za vita ya Majimaji vilivyopigana katika Mikoa nane ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Ruvuma na kuonesha idadi ya mashujaa waliomwaga damu.
Pia Mwakyembe ameshauri Wanafunzi kwenda kujifunza uhalisia wa vitendo,picha mbalimbali na vifaa halisi vilivyotumika katika vita ya Majimaji kwenye Makumbusho ya Taifa ya Majimaji.
Imeandikwa na Netho Credo na Jackline Clavery
Maafisa Habari Serikalini
Agosti 17,2020
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.