Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kukuza sekta za uzalishaji ikiwemo Kilimo, Mifugo na uvuvi kwa lengo la kuzalisha kwa tija na kuongeza fursa za ajira katika sekta hiyo.
Amesema katika kutekeleza hilo, Serikali imeongeza bajeti ya sekta hiyo ambapo Wizara ya Kilimo bajeti imeongezeka kutoka Bilioni 294 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi Trilioni 1.3 mwaka wa fedha 2024/2025.
Mhe. Kikwete alimwakilisha Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya wakulima nanenane Nyanda za Juu Kusini Jijini Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale
Awali akizungumza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnnyeti amesema Wizara ya Mifugo kwa kushirikiana na sekta binafsi inaendelea kutekeleza programu ya mafunzo atamizi ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji kwa vijana ili waweze kujiajiri.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.