Ujenzi wa bandari za Ndumbi na Mbambabay ziwa Nyasa wilayani Nyasa mkoani Ruvuma utatoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuimarisha uhusiano wa kijamii kati ya Tanzania na nchi jirani
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed wakati anazungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea.
Amesema bandari hizo ni sehemu muhimu ya mpango wa kitaifa wa kutengeneza ushoroba wa Mtwara, ambao unatarajiwa kuchochea maendeleo katika mkoa wa Ruvuma na maeneo mengine nchini
Amezitaja nchi za Malawi na Msumbiji kuwa zitanufaika na kwamba bandari hizo zitaongeza uhusiano wa kijamii na kiuchumi kati ya nchi hizo na kuimarisha zaidi uhusiano wa kimataifa.
" Bandari hizi zitawezesha usafirishaji wa abiria kati ya nchi hizo na kusaidia katika masuala ya kiuchumi na maendeleo kwa ujumla.
Kanali Abbas amesema bandari hizo zitafungua milango kwa nchi jirani kutumia miundombinu ya Tanzania kusafirisha bidhaa na kuwezesha usafirishaji wa makaa ya mawe yanayozalishwa kwa wingi mkoani Ruvuma.
Amesema katika utekelezaji wa miradi hiyo,watanzania wanapata faida kubwa ikiwemo kuongeza ajira na kuimarisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, mkoa na Taifa kwa ujumla
Mkoa wa Ruvuma umebarikiwa kuwa rasilimali nyingi yakiwemo madini,hivyo kuwa na miundombinu ya kisasa kama bandari, uwanja wa ndege, na barabara za kuaminika kunatoa fursa kwa wawekezaji kuwekeza hali inatakayochochea maendeleo na kukuza uchumi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.