Wakati mwingine maendeleo hayaji kwa kelele, bali huingia kimya kimya na kuacha alama kubwa.
Hivi ndivyo ilivyotokea kwa barabara ya lami nzito yenye viwango vya kimataifa kutoka Mbinga hadi Mbambabay, mkoani Ruvuma ambayo sasa si tu kiungo muhimu cha usafirishaji, bali pia kivutio cha kipekee kinachowaacha wengi vinywa wazi.
Barabara hii yenye urefu wa zaidi ya kilomita 66, ambayo zamani ilikuwa changamoto kwa wasafiri na wakulima wa maeneo ya Nyasa, sasa imejengwa kwa kiwango cha lami na kugeuka kuwa njia ya kisasa inayoambatana na mandhari ya kuvutia ya milima, mabonde, kuelekea mwambao wa Ziwa Nyasa.
Barabara Inayochora Urembo wa Asili
Ukisafiri kutoka Mbinga kuelekea Mbambabay, ni kama unashuhudia picha halisi ya uzuri wa Tanzania Kusini. Milima ya Livingstone inavyopinda kwa ustadi, mabonde ya kijani kibichi yanavyojaa mazao, na upepo mwanana kutoka Ziwa Nyasa,haya yote hufanya safari isiwe ya kawaida.
“Ni barabara ambayo ukiipitia, huwezi kujizuia kushika simu yako na kupiga picha. Mandhari ni ya kipekee kabisa,” anasema Grace Mkisi, mjasiriamali wa utalii kutoka Songea.
Faida Zaidi ya Kusafiri
Mbali na kuvutia watalii, barabara hii imeleta mapinduzi ya kiuchumi kwa wakazi wa wilaya ya Nyasa. Wakulima sasa wanaweza kufikisha mazao yao sokoni kwa haraka,Pia, huduma za kijamii kama afya na elimu zimeboreshwa kwa sababu ya urahisi wa usafiri.
“Mgonjwa alikuwa akihitaji masaa matano hadi Mbinga Mjini, sasa ni saa moja tu,” anasema Daktari Modest kutoka Kituo cha Afya Mbambabay.
Hongera sana serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kuifungua Wilaya ya Nyasa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.