MENEJA wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga amesema hadi kufikia Juni 30,2023 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa unatekeleza miradi ya maji 36 inayogharimu shilingi bilioni 58.16.
Meneja huyo wa RUWASA alikuwa anatoa taarifa ya utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na RUWASA kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa RUWASA Taifa Mhandisi Ruth Koya kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Madaba Wilaya ya Songea.
Bodi ya Wakurugenzi wa RUWASA Taifa imeanza ziara ya kikazi katika Wilaya za Songea na Mbinga mkoani Ruvuma kwa lengo la kufuatilia miradi inayotekelezwa na RUWASA na kuangalia changamoto mbalimbali zilizopo katika Taasisi ya RUWASA.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.