Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Aziza Mangosongo amewataka watendaji Kata wa Halmashauri ya Wilaya Mbinga kusimamia utekelezaji wa shughuli za lishe katika maeneo yao ili kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa jamii itakayosaidia kuimarisha lishe na kupunguza udumavu nchini.
DC Mangosongo ametoa rai hiyo katika kikao kazi cha tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2023 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
" Suala la lishe ni suala mtambuka kila mtu ana wajibu wa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wetu za kuimarisha lishe na kuondoa udumavu nchini"Amebainisha Mangosongo
Aidha amewapongeza watendaji wa Kata za Kipapa,Ukata,Kihanga Mahuka, Maguu,Mkako, Namswea pamoja na Amani Makolo kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa shughuli za lishe katika maeneo yao,amezitaka Kata zilizobaki kuiga mfano huo ili kuleta matokeo bora zaidi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Sambamba na pongezi hizo DC Mangosongo amewataka watendaji hao kuhakikisha wanahamasisha upatikanaji wa huduma ya chakula kwa wanafunzi shuleni ili kuondoa changaomoto ya mahudhurio hafifu yanayopelekea utoro na hata kukatisha masomo na kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi.
Kwa upande wake Balozi wa Lishe Wilaya ya Mbinga ambae pia ni Diwani wa Kata ya Kitura Mhe. Alex Ngui amewakumbusha watendaji hao kuazimisha Siku za Lishe katika maeneo yao akisisitiza kuwa siku hizo ni muhimu sana katika kuboresha na kuimarisha afya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.