MKUU wa Wilaya ya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo ametoa rai kwa wanawake kuomba mitaji kwa wenzi wao ili kuinua mitaji yao na nkuchangia kuinua uchumi katika familia na jamii kwa ujumla.
Mheshimiwa Mangosongo ametoa rai hiyo katika maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani ambayo katika Mkoa wa Ruvuma kimkoa yatafanyika viwanja vya Bandari Mbambabay wilaya i N yasa ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.
Hata hivyo Mkuu huyo amekemiea tabia ya ukatili wa kijinsia amabazo bado zinaendelea katika jamii yetu , ambapo amesema jukumu la malezi kwa ajamii inatakiwa kusimamiwa na wanawake ambao ndiyo nguzo ya familia.
Kaulimbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka huu inasema “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia chachu katika kuleta Usawa wa Kijinsia”.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.