Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Mheshimiwa Kapenjama Ndile amefanya ziara ya kuzitembelea shule za sekondari zenye wanafunzi wa kidato cha sita katika Manispaa ya Songea kwa lengo la kuwatia moyo kuelekea katika mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika Mei 6 hadi 24 mwaka huu.
Sekondari ambazo Ndile amezitembelea ni shule ya Sekondari Msamala, Dkt. Emmanuel Nchimbi na Sekondari Londoni.
Akizungumza na wanafunzi wa Sekondari hizo kwa nyakati tofauti amewaasa wanafunzi hao kujiamini na kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kuzingatia masomo waliyofundishwa darasani.
Amewatahadharisha wanafunzi hao kutojihusisha na vitendo vya kugushi au kufanya udanganyifu wowote katika mitihani yao hali inayoweza kuwasababisha matatizo.
Mkuu wa Wilaya ametoa kilo 180 za mchele kwa shule tatu za sekondari alizozitembelea sawa na kila shule kilo 60.
Wanafunzi hao wamemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kuwapatia mchele na kuishukuru Serikali kwa kuwajengea miundombinu bora ya shule iliyosababisha wanafunzi hao kusoma katika mazingira ya kuvutia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.