Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mheshimiwa Kapenjama Ndile, amewasihi wanafunzi wa Kidato cha Sita kutoka Shule ya Sekondari Madaba kuwa na nidhamu, kujituma katika masomo na kujiandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.
Akizungumza kwenye mahafali ya 13 ya kidato cha sita yaliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo, Mheshimiwa Ndile amesema elimu ni msingi wa maendeleo ya mtu na taifa, hivyo vijana wanapaswa kuwa mfano mzuri katika jamii.
Alisisitiza kuwa mafanikio hayaji kwa bahati bali kwa bidii na nidhamu ya hali ya juu.
Amewahimiza pia wanafunzi wanaoendelea na masomo Madaba kuhakikisha wanajituma zaidi ili kufikia hatua ya mafanikio ya wahitimu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.