Hifadhi za Wanyama Pori zinazopatikana Mkoa wa Ruvuma zina wanyama wenye tabia ambazo ni mfano wa kuigwa kwa Binadamu.
Akizungumzia Mnyama aina ya Swala mdogo(Digidigi) Afisa Maliasili Msaidizi Kituo cha Taarifa za Utalii Mkoa wa Ruvuma Salum Mussa Baruti amesema mnyama huyo ana tabia ya Upendo wa dhati na uaminifu wa hali ya juu kwa mwenza wake na hupenda kuishi jike na dume.
‘’Endapo dume au jike amekufa anayebaki hataki mwenza tena mpaka anakufa,hao wanyama wana mapenzi ya kweli tofauti na binadamu akifa mwenza wake anaoa au anaolewa tena”,alisema.
Afisa Maliasili Msaidizi huyo amesema wanyama hao aina ya Swala mdogo (Digidigi) kwa Mkoa wa Ruvuma wanapatikana katika hifadhi za Liparamba,Hifadhi ya Taifa Nyerere,Gesimasoa na Litumbandyosi.
Baruti akizungumzia fuvu la Mnyama huyo lililohifadhiwa katika ofisi hiyo amesema Mnyama jamii ya Swala au Digidigi dume anaishi miaka 10 mpaka 16 na jike anaishi miaka 10 mpaka 18.
Hata hivyo amesema Mnyama jamii ya Swala Mdogo au Digidigi anaishi kwenye msitu wenye uoto wa kawaida na chakula anachotumia ni Nyasi pekee hali inayosababisha kuishi mda mrefu.
Amesema mnyama huyo uzao wake wa kwanza kwa mwaka mmoja anazaa mara moja na kadri anavyoendelea kwa mwaka unaofuata huzaa mara mbili kwa mwaka na anabeba mimba kwa miezi mitano na kuzaa mtoto mmoja tu.
Baruti ameitaja sifa ya Mnyama huyo kuwa ana uwezo wa kuona vizuri usiku na mchana na Jike hana pembe lakini ana mwili mkubwa,dume ana pembe mbili na ana mwili mdogo.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Afisa Habari Halmashauri Ya Madaba
Novemba 11,2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.