HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba inamaeneo mazuri ya Uwekezaji wa Viwanda pamoja na Uwekezaji wa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na Biashara.
Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Kassim Mpenda amesema anawakaribisha wawekezaji katika Halmashauri ya Mdaba kwakuwa Ardhi ya Madaba inafaa kwa kilimo cha mazao ya Biashara,chakula na Viwanda.
‘’ kufikia Juni 2019 Halmashauri hiyo ilikuwa na wawekezaji wakubwa wa 4, Silverland Ndolela anafanya shughuli za kilimo cha mazao na ufugaji eneo la Hekta 5,000,Wakala wa misitu Tanzania (TFS)anafanya shughuli za upandaji wa miti eneo la vijiji vya ifinga Wino na Mkongotema zaidi ya Hekta 24,000,Chuo kikuu cha Sokoine Hekta 10,000 kijiji cha Ifinga wamepanda miti zaidi 2,000,Mbangamawe partiners anazalisha chokaa katika kijiji cha Mtyangimbole”.
Aidha amesema Mwekezaji wa kampuni ya Ifinga food processing anaongeza thamani ya mazao kwa kufungasha kama Tangawizi,na Mwekezaji mwingine Kampuni ya Interfruit Limited ya Mjini Songea inatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha matunda ya Parachichi Hekari 3,000 na kujenga Kiwanda cha kusindika matunda mara yatakapoanza kuvunwa katika kijiji cha Mahanje.
Vile vile Mkurugenzi amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mdaba inazalisha mazao ya kilimo kama Miti ya Mbao,fito,nguzo za umeme/simu,kilimo cha Kahawa,Tangawizi,Matunda,Mpunga na Mazao ya Mafuta.
“Matarajio ya Halmashauri ni kupokea wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya kilimo na umwagiliaji ili watumie maeneo mazuri yaliyopo kwenye eneo letu,Kuwapokea wawekezaji wa kujenga viwanda vya kuchakata mazao ya misitu(Miti) na Nafaka Mahindi)”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo akielezea maeneo yanayotambulika kwa kuwekeza amesema Kitongoji cha Ifungwa kijiji cha Madaba kilo mita 10 kutoka Barabara kuu Songea- Njombe kina Hekari 400 eneo hilo limetengwa kwaajili ya Uwekezaji wa Kiwanda au shughuli yoyote kwa kuwekeza katika eneo hilo.
Amesema eneo la Itombolo lina Hekta 2000 lipo katika Kijiji cha Mkongotema mpakani na kijiji Lutukila kandokando ya Barabara kuu ya Songea-Njombe ni eneo lililotengwa kwaajili ya shughuri ya Viwanda vya kuchakata mazao ya Mahindi,Tangawi na Mzao Mengine, eneo hilo ni mali ya Kijiji Halmashauri na Kijiji watahakikisha Mwekezaji anapata Eneo analihitaji ili wananchi wanufaike na fursa na kazi zitakazoendelea eneo hilo.
Akiendelea kuelezea maeneo ya kuwekeza katika Halmashauri hiyo amesema kuna Hekta 4,200(Hekari) ni shamba la Mifugo na ni Mali ya Wizara ya Mifugo lipo kando ya Barabara kuu Songea-Njombe,Halmashauri ya Madaba inatunza na kulitumia amesema Wawekezaji wanakaribishwa kwaajili ya shughuri ya ufugaji mifugo ya (Ng’ombe),kwa sasa kuna wafugaji waliokodishwa vitalu 16 na bado kuna nafasi ya vitalu 8 na eneo limepitiwa na mto mkubwa unaowezesha kutumika kwa uzalishaji wa chakula cha Mifugo.
“Halmashauri ya Wilaya ya Mdaba inamiliki eneo lenye Hekari 500 lipo km 18 kutoka Barabara Kuu Songea Njombe ukielekea Kijiji cha Ifinga na eneo Hilo lipo tayari kwaajili ya mwekezaji kuwekeza kwa shughuli za kilimo hasa kilimo cha Miti,Kahawa,na Mazao mengine yanayoendana pamoja na maporomoko ya Umeme Masigira,Lipupuma,na Lingatunda”.
Pia Halmashauri ya Madaba na vijiji vyake 21 inamaeneo ya kutosha hivyo yeyote anakaribishwa kuwekeza katika maeneo hayo na vijiji 11 vimepimwa Halamashauri itahakikisha mwekezaji anapata eneo la kutosha analohitaji katika kijiji chochote kwa kilimo cha mazao.
Halmashauri ya Madaba inatoa rai kwa wawekezaji kuwekeza katika Viwanda mbalimbali kwenye mji wa Madaba na Vijijini ikiwa tayari vijiji 19 vinaumeme wa uhakika,kutokana na malighafi zilizopo Viwanda vya uchakataji wa Mazao ya Misitu na Usindikaji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Halmashauri ya Madaba
Novemba 24,2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.