Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Mhe.Mennas Komba ametoa onyo kwa Watendaji na Viongozi wa Halmashauri hiyo kukumbatia migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali.
Mhe. Komba ametoa onyo hilo katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo katika kijiji cha Lundusi.
Mhe.Komba ametoa onyo hilo kufuatia kuripotiwa matukio ya migogoro baina ya wakulima na wafugaji inayoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri.
“Nimepokea ujumbe kwanjia ya simu wananchi wanalalamika kuhusu uwepo wa ngo’mbe katika maeneo ambayo ni ya wakulima”,amesisitiza Mhe.Komba.
Kufuatia kadhia hiyo Mhe.Komba ameahidi kwenda katika maeneo ambayo yanamigoro kwa lengo la kufanya mikutano ya hadhara ili kubaini ukweli wa chanzo cha migogoro hiyo na kuitafutia ufumbuzi.
Kwa upande mwingine Halmashauri ya Wilaya imeshakwisha tenga maeneo kwa ajili ya kupima vitalu na kuvigawa kwa wafugaji kwaajili vya kuchungia mifugo yao katikaVijiji vya Magwamila,Lugagara,Litowa,Mhepai na Nambendo,ambavyo vitatolewa kwa mfugaji yoyote anayehitaji kwa masharti ya kukidhi vigezo kwa mujibu wa taratibu na sheria za Nchi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.