Huduma ya maji maeneo ya vijijini katika Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma imepanda na kufikia asilimia 62 ndani ya kipindi cha miaka minne.
Kaimu Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Mbinga Mhandisi Frolian Francis amesema miaka minne iliyopita, huduma ya maji vijijini ilikuwa ni asilimia 49 tuu.
Amesema mafanikio hayo yanakuja kutokana na zaidi ya miradi 15 inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Mbinga .
“miradi hii yenye thamani ya shilingi bilioni 17 itakapokamilika, huduma ya maji vijini itafikia asilimia zaidi ya 85 hadi kufikia mwaka 2025,” alisisitiza Mhandisi huyo wa maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.