Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amesema Serikali imefanya Maboresho makubwa katika sekta ya elimu katika kipindi cha miaka mitatu.
Kauli hiyo ameitoa Wakati alipoongozana na Wenyeviti wa Mashina wa CCM katika kata ya Parangu, Mpandangido, Kilagano na Maposeni kujionea utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwenye ujenzi wa Miundo Mbinu ya Mambweni na Madarasa uliyofanyika katika shule ya sekondari Maposeni na Mtopesi katika Halmashauri ya Songea Mkoani Ruvuma.
Waziri Mhagama amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza Rais Samia imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, ili kupunguzia wananchi adhaa ya kuchangishana michango kwa ajili ya ujenzi.
Katika shule ya Sekondari Maposeni kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 40, ambapo kuna madarasa ambayo ujenzi umekamilika na mengine yako mbioni kujengwa.
"Hivyo basi jamii inawajibu wa kumlinda mtoto wa kike na kumlinda mtoto wa kiume kwa kuwapatia elimu bora itakayosaidia kujenga Jamii yenye weledi," alisema.
Ameongeza kusema zawadi nyingine aliyotupatia Rais ni kuhakikisha anafuta ada na kusaidia watoto wengi kwenda shule.
"Kutokana na ongezeko la wanafunzi, tunahitaji kuongeza miundo mbinu ya elimu kwa ajili ya vijana wetu, Serikali inaandaa mitaala mpya ambayo itasaidia kuwapa elimu ya ufundi vijana wetu waweze kupata ujuzi " alibainisha
Sambamba na hilo Halmashauri ya Songea Vijijini, serikali itajenga chuo kikubwa cha Ufundi cha VETA katika Kata ya Liganga ili kuwezesha vijan kupata elimu ya ujuzi katika chuo hicho.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Vijijini Menace Komba amesema tayari wameshaanza utaratibu wa kuomba wizara ya elimu ili kupata kibali cha kubomoa majengo ya zamani ya shule ya sekondari Maposeni na Mpitimbi ili kujenga Madarasa mapya.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.