Kamati ya Lishe katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imeweka utaratibu wa kutoa Elimu ya afya na lishe kwa vitendo kwa wazazi wenye watoto chini ya miaka mitano.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Afisa Elimu Msingi katika Manispaa hiyo Frank Sichalwe imedhamiria kuondoa utapiamlo na udumavu.
Akizungumza siku ya afya na lishe iliyofanyika katika Mtaa wa Likuyufusi kata ya Lilambo Manispaa ya Songea,Sichalwe amewataka wazazi na walezi kutumia vyakula vyenye viini lishe kwa Mama mjamzito ili kusaidia maendeleo ya ukuaji ya mtoto.
“Wazazi wanatakiwa kufanya usafi katika mazingira yanayowazunguka ili kuepukana na magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira yakiwemo malaria, mafua, kuhara pamoja na kipindupindu’’,alisema.
Naye Afisa Lishe Manispaa ya Songea Alberth Semkamba Ametoa rai kwa jamii kuzingatia umuhimu wa siku 1000 za mwanzo za mtoto kuanzia utungaji mimba hadi kuzaliwa kwa mtoto.
Amesisitiza kuwa katika kipindi hicho mtoto atatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya Mama pekee hadi pale tu atakapofikisha umri wa miezi sita.
Kaulimbinu ya siku ya afya na lishe mwaka huu inasema lishe bora kwa afya na maendeleo kwa kizazi kijacho
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.