Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria imefanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa stendi ya mabasi unaotekelezwa na mfuko wa TASAF wenye thamani ya zaidi ya shilling milioni 400 katika kijiji cha Lundusi kata ya Peramiho Wilaya ya Songea.
Ziara hiyo, imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Katiba na Sheria Dkt Joseph Mhagama.
Dkt Mhagama amempongeza Mkurugenzi wa TASAF na timu yake kwa usimamizi mzuri wa mradi huu kwa namna bora sana.
“ Nimpongeze sana mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kipaumbele kikubwa sana kwa maendeleo ya wana Peramiho”, amesema Mhagama.
Dkt Mhagama amesema Mheshimiwa Rais amefanya jitihada kubwa kupeleka huduma mbalimbali za kijamii karibu na wananchi.
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesema ujenzi wa kituo hicho unamhakikishia Mkurugenzi uongezaji mapato.
Kikwete amesema stendi hiyo itafungua fursa kubwa kwa wakazi wa Wilaya hiyo kwa kufanya biashara tofauti ambazo zitawaingizia kipato.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma Komredi Oddo Mwisho amesema mradi huu wa TASAF una manufaa makubwa kwa wananchi.
Mhandisi wa Ujenzi Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhandisi Flora Tairo amesema katika mradi wa ujenzi wa mradi wa stendi hiyo walipokea zaidi ya shilingi millioni 400 za utekelezaji wa mradi huo ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi milioni 270 zimetumika kutekeleza mradi huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.