MADAKTARI Bingwa wa kambi ya matibabu ya kibingwa ya afya ya akili wanatoa huduma za matatibu kwa siku tano kuanzia Desemba 16 hadi 20 mwaka huu.
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kambi hiyo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea,alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano.
Akizungumza kwenye ufunguzi huo Mbano ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa jitihada kubwa wanazofanya katika kuhakikisha huduma za afya ya akili zinatolewa kwa wananchi.
“Nimefurahishwa na juhudi za kutoa huduma za matibabu ya afya ya akili. Idadi ya wagonjwa wa nje na wale wa kulazwa mnaowahudumia inaonesha kuwa hitaji la huduma hizi ni kubwa, hasa kwa magonjwa yanayoongoza kama vile msongo wa mawazo,( Schizopherenia ) na matatizo ya utumiaji wa dawa za kulevya’’,alisema.
Amesema Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Kupitia Wizara ya Afya imeweka kipaumbele cha tisa Katika kuimarisha huduma za afya ya akili.
Hata hivyo amelitaja lengo ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi, bila kujali mazingira yake, anapata huduma bora ya afya ya akili na kwamba huduma tembezi ni moja ya mikakati madhubuti inayolenga kufanikisha azma hiyo.
Amesisitiza kuwa madaktari Bingwa ya afya ya akili waliopo mkoani Ruvuma hawatasaidia tu kutoa huduma kwa wagonjwa, bali pia wataongeza maarifa kwa watoa huduma kupitia mafunzo na kubadilishana uzoefu.
Ametoa wito kwa watoa huduma wote kuendelea kuwa na moyo wa kujituma, kujifunza, na kushirikiana kwa ukaribu na madaktari bingwa wa afya ya akili.
Naye Daktari Bingwa wa Afya ya Akili kutoka Hospitali ya Taifa Dodoma Dr. Sadiki Mandaru amesema hii ni kambi ya pili kufanyika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambapo kambi ya kwanza ilifanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Ametaja moja ya uchunguzi wa afya ya akili ambao utapewa kipaumbele ni Pamoja na uchunguzi wa Sonona, wasiwasi uliopitiliza, matumizi ya dawa za kulevya,na kutoa ushauri wa kisaikolojia, na kimatibabu.
Amesema madaktari bingwa hao pia watafanya kipimo kikubwa cha umeme wa ubongo ambacho ni maalum kwa watu wenye ugonjwa wa kifafa.
Kwa upande wa Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Songea Dr. Magafu Majura, amewashukuru Madaktari bingwa wa afya akili kwa ujio ambao wamesema watasaidia kutoa matibabu kwa watu wenye changamoto za afya ya akili.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.