Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo ameitembelea na kuikagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Songea (HOMSO) ambapo amewapongeza watumishi kwa huduma bora wanazozitoa kwa wananchi.
Amewataka watumishi wa afya kuhakikisha wanatoa huduma bora, kudumisha nidhamu kazini, kuwajibika na kuzingatia uadilifu kwa ajili ya kuwahudumia Watanzania.
"Wajibu wetu ni kuhakikisha kwamba tunawapatia huduma bora, tunazingatia uwazi, tunatekeleza wajibu wetu kwa uadilifu tukijituma zaidi kwa ajiri ya kuwahudumia Watanzania na Wanaruvuma". alisema.
Amewahimiza watumishi wa afya kuwa na utumishi uliotukuka, huku wakitoa huduma bora na kuzingatia mahusiano mazuri kati yao na wagonjwa.
Ameeleza kuwa ni heshima kubwa kwa watumishi wa afya kutekeleza majukumu ya kuhakikisha afya za wananchi zipo katika hali njema ili waweze kuchangia uchumi na shughuli za kijamii.
Amebainisha kuwa Serikali inatambua changamoto za watumishi wa afya, hasa madai ya malipo, na inayafanyia kazi changamoto hizo ili kuhakikisha wanapata stahiki zao.
Ameahidi kuendelea kushirikiana na hospitali hiyo ili kuhakikisha changamoto zinazowakabili watumishi wa afya zinatatuliwa huku akiahidi kuandaa siku maalum atakayozungumza nao kwa kina.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa hospitali 28 za Rufaa zilizopo nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.