Pichani ni Katibu Tawala Wilaya ya Tunduru Ndg. Milongo Sanga ( mwenye kofia ) akishiriki chakula cha jioni Novemba 12, 2023 pamoja na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Masonya ambao wameanza Mtihani wao wa kidato cha Nne Novemba 13, 2023
Katibu Tawala aliwatia moyo na kuwatakia kheri wananfunzi hao wa kidato cha nne katika Mtihani wao wa kidato cha nne wa kuhitimu Elimu ya Sekondai
iAidha Afisa Elimu Sekondari (W) Tunduru Ndg.Patrick Haule aliwatakia kheri katika Mtihani huo wa Taifa pia amewasisitiza kushika yale waliofundishwa na kuweza kujibu Mitihani yao kwa umakini.
Shule za sekondari 23 kati ya shule 29 zimeanza kufanya Mtihani wa kidato cha nne leo Novemba 13, 2023, ambapo shule 21 ni shule za Serikali na shule 02 ni shule za Binafsi, ambapo jumla ya watahiniwa 1,882 wamesajiliwa kufanya Mtihani huo wa Taifa ikiwa Wavulana 904 na Wasichana 978.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.