Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025, Ismail Ally Ussi, ametoa onyo kali dhidi ya vitendo vya rushwa, akisisitiza kuwa ni tishio kwa demokrasia, haki na maendeleo hasa katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wilayani Songea, mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika viwanja vya Shule ya Msingi Igawisenga, Halmashauri ya Madaba, Ussi alitoa ujumbe mzito kwa viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi, akiwataka kujitenga kabisa na vitendo vya rushwa vinavyoweza kuhatarisha uchaguzi huru na wa haki.
“Rushwa ni adui mkubwa wa haki na uwajibikaji. Ni lazima tupambane nayo kwa nguvu zote ili kulinda misingi ya uchaguzi wa kidemokrasia,” alisisitiza Ussi huku akihimiza mshikamano wa kitaifa katika kuikataa.
Katika ziara hiyo ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo, Ussi aliwataka Watanzania kuwa walinzi wa maadili na kuhakikisha kuwa kila hatua ya mchakato wa uchaguzi inazingatia uwazi na uadilifu, bila kuruhusu ushawishi wa kifedha au upendeleo.
Ussi alihitimisha kwa kueleza kuwa Mwenge wa Uhuru si tu alama ya historia, bali pia ni mwanga wa kupambana na maovu kama rushwa, akitoa rai kwa kila mmoja kuenzi ujumbe huo kwa vitendo ili kudumisha amani, umoja na maendeleo ya kweli.
Mwenge wa Uhuru upo mkoani Ruvuma hadi Mei 17 utakapokabidhiwa katika Mkoa wa Mtwara
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.