Mbunge wa jimbo la Tunduru Kaskazini, mkoani Ruvuma Mheshimiwa Hasani Zidadu Kungu, amefungua rasmi Kituo cha Afya Juma Homera kilichojengwa katika Kata ya Nakayaya mjini Tunduru
Kituo hicho sasa kimeanza kutoa huduma kwa wananchi baada ya kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wake.
Ujenzi wa kituo hicho umegharimu zaidi ya shilingi milioni 400, fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Fedha hizo zilitumika kukamilisha majengo na kununua vifaa vya tiba ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Historia ya mradi huo inahusiana na jitihada za aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Mheshimiwa Juma Homera, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Mheshimiwa Homera aliratibu upatikanaji wa rasilimali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na kuunda kamati za usimamizi wa ujenzi.
Baada ya kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa kituo hicho, kimefunguliwa rasmi kwa matumizi ya wananchi.
Hii ni hatua kubwa katika kuimarisha sekta ya afya katika wilaya ya Tunduru na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa ukaribu zaidi.
Kupatikana kwa kituo hiki kutapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali kubwa na kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa maeneo ya jirani.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.