Mkuu wa Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mheshimiwa Aziza Mangosongo amekabidhi gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) katika kituo cha afya Kindimbachini.
Mangosongo pia amekabidhi madawati 179 pamoja na vifaa vya kujifunzia katika shule za Msingi 10 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Hafla Makabidhiano hayo imefanyika katika viunga vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mangosongo ameutaka uongozi wa shule zilizokabidhiwa madawati na vifaa hivyo kuhakikisha vinatunzwa vizuri ili vitumike kwa muda mrefu.
" Serikali imetuletea vifaa hivi ni jukumu letu kuhakikisha tunavitunza, nitashangaa kuona vifaa hivi vimeharibiwa utakuwa ni uzembe mkubwa sana" Alisema Mangosongo
Hata hivyo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Juma Haji kwa kutekeleza agizo la kutengeneza madawati ili kukabiliana na upungufu wa madawati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Juma Haji amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta gari la kubebea wagongwa katika kituo cha afya Kata ya Kindimbachini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.