Maandalizi ya Tamasha la utamaduni la tatu kitaifa linalotarajiwa kufanyika Septemba Mwaka huu katika uwanja Majimaji Mkoani Ruvuma yaendelea kushika Kasi ngazi ya Mkoa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Tamasha hilo ambapo anatarajiwa pia kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amefungua kikao cha maandalizi ya Tamasha hilo kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Akizungumza wakati akifungua kikao hiko Mkuu wa Mkoa amesisitiza kujiandaa vyema na kuhakikisha watu wanajitokeza kwa wingi katika Tamasha hilo.
"Nawaomba kwa imani zetu, tumtangulize Mwenyezi Mungu kulifanya jambo hilo liwe na mafanikio makubwa kusitokee changamoto ambayo inaweza ikatia dosari ziara hiyo ambayo kwetu ni heshima kubwa", alisema.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Mary Makondo amesema kimkoa tayari kazi kubwa ya maandalizi ya tamasha imeshafanyika na wanaaendelea kushirikiana na Wizara yenye dhamana ili kuhakikisha tamasha linafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.