AFISA Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Ruvuma Mariam Juma ametoa Elimu ya mpango wa Taifa ya Malezi na makuzi ya awali ya Mtoto katika Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
Akizungumza katika Baraza hilo amesema mpango huo unasimamiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii jinsia wanawake na makundi maalum na ulizinduliwa na Waziri Doroth Ngwajima Desemba 2021 mjini Dodoma.
Amesema Mpango huo unafanyika katika Mikoa yote 26 ukiwemo Mkoa wa Ruvuma ulianza kutekelezwa mwaka 2022 ikiwa ni mpango wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi 2026.
Juma amelitaja lengo la mpango huo kuwa ni kutoa huduma ya afya, lishe , malezi yenye mwitikio,ujifunzaji wa awali kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0-8 na kuimarisha ushirikiano kwa wadau katika sekta mbalimbali na kutoa huduma za mama.
“Ukuaji wa mtoto unaanza tangu anapokuwa tumboni hivyo wazazi na Serikali tunajukumu la kuhakikisha chanjo zote zinapatikana,malezi yenye mwitikio kuzungumza na mtoto anapokuwa tumboni,lishe bora na ujifunzaji wa awali”.
Hata hivyo amesema asilimia 90 ya ya ukuaji wa mwanadamu inatengenezwa kuanzia miaka 0-8 na asilimia 10 inatengenezwa kuanzia miaka 8 na kuendelea .
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.