Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wa Kamati ya Fedha na Uongozi wamekagua miradi sita ya maendeleo yenye thamani ya Zaidi ya shilingi bilioni moja.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Naibu Meya Manispaa ya Songea Mheshimiwa Jeremiah Mlembe wametembelea na kukagua miradi hiyo ambayo ni ujenzi wa madarasa mawili na matundu manne ya vyoo shule ya msingi Ndilima litembo inayojengwa kwa kiasi cha fedha Milioni. 54,800,000, Ujenzi wa madarasa saba sekondari ya Mdandamo yanayogharimu shilingi Milioni. 170,500,000 na Ukamilishaji wa Hospitali ya Manispaa ya Songea inayojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 800.
Miradi mingine ni ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi inayojengwa kwa gharama ya Mil. 180,000,000, ujenzi wa madarasa10 na matundu 10 ya vyoo shule ya Sekondari Londoni kwa kiasi cha Mil. 259,500,000 na Ujenzi wa vyumba vya madarasa 8 shule ya Sekondari Sili kwa kiasi cha 192,000,000.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.