Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, imeamua kuboresha lishe kwa shule za msingi pamoja na sekondari katika halmashauri hiyo.
Kupitia taarifa ya kikao cha lishe na utekelezaji, kilicho fanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea, ambapo kimewakutanisha wadau wa lishe, ambao wameamua shule za bweni na za msingi ziongezewe lishe bora.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Dkt Frederick Sagamiko, ameeleza namna Manispaa hiyo ilivyoweka mikakati ya kuboresha lishe kwa wanafunzi wa Manispaa hiyo kwalengo la kupunguza matatizo ya mtapia mlo kwa wanafunzi.
“Kimsingi tumekubaliana tunahitaji kuona matokeo makubwa zaidi kwa wananchi tunao wahudumia, zile changamoto zinazo ripotiwa kama mpatia mlo hivyo vyote tunatakiwa kuviondoa, lakini tumekubaliana shule zetu ziweze na bustani na tumekubaliana tuwe na kituo kimoja cha maziwa” alisema Sagamiko.
Naye Afisa lishe Manispaa ya Songea, Kisaka Joseph, ameeleza maadhimiyo ya kikako hicho kwamba shule zote za bweni na shule za msingi, kuhakikisha wazabuni wote wanaopeleka vyakula shuleni, wahakikishe vyakula hivyo viwe na ongezeko vya viini lishe.
“Kwahiyo kikao kimeridhia shule zote za bweni na msingi zilizopo manispaa, ziwe na bustani kwa maana ya upatikanaji wa mboga mboga mashuleni na kuna aina nyingi za bustani ambazo zinahitaji eneo dogo zipo bustani viroba, bustani machupa hizo zote hazihitaje eneo kubwa” alisema Joseph.
Hata hiyo idara ya mifugo na vuvi ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea, imepewa maagizo ya kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa kuhimalisha vikundi vya wafugaji vilivyopo na kufuga kisasa ili kuzalisha maziwa kwa wingi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.