MANISPAA ya Songea imeongoza kwa Ufaulu wa Darasa la Saba mwaka 2021 kwa asilimia 88.019.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Hakimu Mafuru amezungumza ofisini kwa amesema wanafunzi wa Darasa la saba wapatao 39,614 walisajiliwa kufanya mtiahani wa wa darasa la saba.
Amesema wanafunzi waliofanya mtihani wa kumaliza Elimua ya Msingi walikuwa 39,604 sawa na asilimia 99.9 na waliofaulu mtihani walikuwa 28,356 sawa na asilimia 73.1 walifanikiwa kujiunga na kidato cha kwanza.
“Katika Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma Manispaa ya Songea ilichukua nafasi ya kwanza kwa kufaulisha wananfunzi 5,172 sawa na asilimia 88.019”.
Mafuru amesema Halmashauri iliyofutia ni Madaba kwa kufaulisha wanafunzi 1,139 sawa na asilimia 86.288 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Halmashauri ya Nyasa kwa kufaulisha wanafunzi 3,430 sawa na asilimia 75.734.
Hata hivyo amesema hali ya Samani katika Shule za Msingi hadi kufikia Machi 2022 Mkoa unamahitaji ya madawati 126,248 yaliyopo 102,430 na upngufu ni 23,818.
Amesema Mkoa kwa kushirikiana na Wilaya zake umeendelea na jitihada mbalimbali ili kuweza kuondoa upungufu uliopo.
Afisa Elimu amesema Hali za majengo katika Shule za Msingi Mkoa unauhitaji wa wa vyumba vya Madarasa 10,003 yaliyopo ni 6,294 na upungufu ni 3,709 .
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 12,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.