WANANCHI mkoani Ruvuma Oktoba 19 mwaka huu wanatarajia kupata burudani ya aina yake ya soka baada ya timu ya Yanga kutumia uwanja wa Michezo wa Majimaji kukabiliana na Timu ya KMC kwenye michuano ya ligi kuu ya Tanzania bara.
Akizungumzia mchezo huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ametoa rai kwa wananchi mkoani Ruvuma na mikoa ya jirani kufika kutazama mchezo huo wa ligi kuu ambapo amesisitiza hali ya ulinzi na usalama mkoani Ruvuma ni nzuri.
Ametoa rai kwa watoa huduma wote kuendelea kutoa huduma bora kwa wageni wote ambao wameanza kuingia kwa ajili ya kutazama mechi ya Yanga na KMC.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewatahadharisha wananchi wanapokuwa kwenye misongamano ya watu kama uwanjani kuchukua tahadhari dhidi ya UVIKO 19 kwa kuvaa barakoa,kukaa umbali za kuanzia meta moja na kutumia vipukusa mikono au maji tiririka kwa sabuni
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa amewaalika wageni wote ambao watakuwa mkoani Ruvuma katika kipindi hiki cha kutazama soka pia kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo mkoani Ruvuma vikiwemo ziwa Nyasa,Makumbusho ya Taifa ya Majimaji,Chanzo cha Mto Ruvuma ,Hifadhi ya Taifa ya Nyerere na maeneo mengine ya historia
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.