Maporomoko ya Nakatuta Mto Ruvuma ndani ya pori la Akiba Liparamba wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ni moja ya vivutio vya aina yake vinavyopamba pori hilo ambalo pia lina wanyama,mimea na ndege wa aina mbalimbali.
Maporomoko ya Mto Ruvuma katika eneo la Tulila mpakani mwa Wilaya za Songea na Mbinga ni moja ya kivutio cha uwekezaji na utalii ambapo watawa wa Shirika la Mtakatifu Agnes Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea wamewekeza katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia nguvu ya maji ya mto Ruvuma.
Muonekano wa Mto Ruvuma wilayani Namtumbo.Mto Ruvuma ambao umeanzia milima ya Matogoro Manispaa ya Songea,umepita katika wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma kuanzia Songea,Mbinga,Nyasa,Namtumbo hadi Tunduru na kumwaga maji yake Bahari ya Hindi mkoani Mtwara.Mto Ruvuma una urefu wa zaidi ya kilometa 800,ni miongoni mwa mito mirefu barani Afrika.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.