MSEMAJI wa familia ya Marehemu Florence John Nyingo kupitia kwa Mdogo wa Marehemu Nestory John Nyingo amesema familia imesitikishwa na taarifa ambazo sio sahihi zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ndugu yao alifariki baada ya kuzidiwa akiwa kwenye foleni ya mbolea ya ruzuku katika duka la Mohamed Enterprise mjini Songea.
Akizungumza kwenye mkutano wa wanahabari mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema,mdogo wa Marehemu amesema Marehemu kaka yake alikuwa na matatizo ya kiafya na alizidiwa akiwa ametoka nyumbani kwao Nakahuga Wilaya Songea na alipofika naye stendi ya Mfaranyaki mjini Songea alizidiwa na kuishiwa nguvu na kwamba alikodi pikipiki na kumkimbiza hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma ambako alifariki wakati anaendelea kupata matibabu..
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mheshimiwa Pololet Mgema amewaambia wanahabari kuwa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari sio sahihi,hazikufanyiwa utafiti na zinastahili kukanushwa ili watanzania wapate taarifa sahihi.
Hata hivyo ameipongeza serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mbolea ya ruzuku kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula.
Amesema serikali wilayani Songea inaendelea kushughulika changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa Mfumo wa mbolea ya ruzuku ambao wakulima wengi wananufaika nao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.