WILAYA ya Nyasa mkoani Ruvuma imebarikiwa kuwa na fukwe za asili ambazo hazifanani na fukwe nyingine zozote duniani na endapo zitaendelezwa zinaweza kuwa chanzo muhimu cha mapato katika wilaya ya Nyasa
Wananchi wa mikoa ya kusini ukiwemo mkoa wa Ruvuma bado hawajanufaika katika sekta ya utalii moja ya sababu kubwa ni kwamba wananchi wa mikoa ya kusini hawajapata elimu sahihi kuhusu utalii na faida zake.
Mwenyekiti wa Mtandao usio wa Kiserikali wa Mkoa wa Ruvuma RUNECISO Michael Mahecha ametoa wito Wananchi na wadau mbalimbali kuziendeleza fukwe zilizopo ili kuwavutia Watalii wa Ndani na Nje ya Nchi.
Mwenyekiti huyo ameyasema wananchi wa maeneo ya mwambao mwa ziwa Nyasa kushindwa kutumia fursa za utalii zilizopo badala yake wamekuwa mstari wa mbele kuuza Fukwe kwa wageni wanaofika kutoka nje ya wilaya hiyo.
MILANGO ya utalii mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma inaendelea kufunguka ambapo sasa serikali inatarajia kuanzisha bustani ya wanyamapori katika Milima miwili na visiwa viwili vilivyopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
Kutokana na hali hiyo Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma anasema tayari mchakato wa kuendeleza Mbamba Hill iliyopo mjini Mbambabay Makao makuu ya Wilaya ya Nyasa kuwa hifadhi ya wanyama unaendelea vizuri na kwamba ya tayari bajeti imepitishwa.
“Tumeshapima eneo lote la Mbamba Hill,ina ukubwa wa hekta 420,ndani ya hifadhi hiyo kuna wanyama kama nyani, nyoka, pimbi,chui na ndege wa aina mbalimbali’’, anasema Challe.
Challe anabainisha kuwa hifadhi hiyo imeunganishwa na kisiwa kinachoitwa Zambia ambacho kipo meta 300 toka ufukweni mwa ziwa Nyasa na kwamba kisiwa hicho kina utajiri wa aina mbalimbali za samaki wa mapambo ambao ni kivutio cha watalii.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.