Kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani ya Halmashauri ya Mji Mbinga imesema mambo tisa yatafanyika kuelekea, na wakati wa maadhimisho ya siku hiyo itakayofanyika Oktoba Mosi mwaka huu.
Mwenyekiti wa Maandalizi ya maadhimisho ambaye pia ni Afisa Ustawi wa Halmashauri ya Mbinga Mji Lucas Muhina ameyataja Mambo hayo ni kutoa huduma za afya yakiwemo matibabu, vipimo na elimu lishe kwa wazee, kutoa msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa wazee na wananchi wenye uhitaji na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya maadili na ukatili.
Amesema katika maadhimisho hayo zitatolewa huduma za ustawi kwa wazee na kutoa elimu kuhusu huduma za ustawi wa jamii hususani kwa wazee katika vyombo vya habari na mikutano.
“Sanjari na hayo, wadau watajadili namna bora ya kutatua changamoto za wazee, kudhibiti mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia, na kupata shuhuda za vitendo vya ukatili dhidi ya wazee vilivyowahi kutokea katika maeneo mbalimbali,” alisema Bw. Muhina.
.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.