Hakuna ubishi Mji wa Mbambabay uliopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma utafufuka kwa kasi kutokana na kukamilika kwa mtandao wa barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbambabay na kitendo cha serikali kununua meli tatu mpya kati ya hizo meli mbili za MV Njombe na MV Ruvuma ni za mizigo na meli moja ya MV Mbeya II ni ya abiria.
Kulingana na Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA meli zote tatu zimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 20.1 ambazo zimetolewa na serikali kujenga meli kwa kutumia kampuni ya Songoro Marine inayomilikiwa na Mtanzania.
Meli mbili za mizigo MV Njombe na MV Ruvuma kila moja ina uwezo wa kubeba tani 1000 na kwamba kila meli imegharimu shilingi bilioni 5.5 na meli ya abiria ya MV Mbeya II ina uwezo wa kubeba abiria 300 na mizigo tani 200, imegharimu shilingi bilioni 9.1.
Kwa mujibu wa TPA meli ya abiria ya MV Mbeya II imerithi jina la meli ya MV Mbeya I iliyozama eneo la Makonde ziwa Nyasa mwaka 1977.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.