Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jeneralii Wilbert Ibuge ametoa rai kwa wananchi kuendelea kupokea Elimu na kuchanja kwa hiari kwa lengo la kupunguza madhara na changamoto ya ugojwa wa UVIKO -19.
RC Ibuge ametoa rai hiyo katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Mkoa kuhusu chanjo ya UVIKO 19 kilicho fanyika Oktoba Mosi katika ukumbi wa Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa ametoa rai kwa wananchi kuchanja kwa hiari kwa sababu chanjo ya UVIKO -19 ina umuhimu mkubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo,gharama kubwa ya matibabu endapo mtu atapata maambukizi ya ugonjwa wa UVIKO -19 na mrundikano wa wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya.
RC Ibuge amewapongeza wananchi wa mkoa wa Ruvuma kwa kupokea elimu kuhusu umuhimu wa chanjo na kuchanja kwa hiari kitendo ambacho kinatoa fursa ya mapambano dhidi ya UVIKO -19 ambao ni nitishio kwa maisha na uhai wa binadamu.
Amezitaja baadhi ya changamoto ambazo zinasababisha wananchi kutohiari kuchanja kuwa ni kutokuwa na elimu sahihi ya faida za chanjo,watu maarufu kutoa maelekezo hasi kwenye jamii kuhusu umuhimu wa chanjo na baadhi ya viongozi wa dini kutotoa ushirikiano katika zoezi la uhamasishaji wa chanjo.
Amesema mkoa wa Ruvuma kwa kipindi cha siku nane kupitia mpango wa huduma shirikishi na harakishi umefanikiwa kuchanja jumla ya watu 21,303 sawa na asilimia 82 kutokana dozi 25,000 ambazo mkoa ulikuwa nazo hadi kufikia Septemba 30,2021.
“Janga lililo mbele yetu ni kupoteza maisha ,shida ya kuchanja wachache ni kuambukiza wengi,na kuchanja wengi ni kupunguza maambukizi,” amesisitiza Balozi ibuge.
Naye Katibu wa Cha Mapinduzi wa Mkoa wa Ruvuma Nelly Ngeleja ametoa wito kwa wananchi kushikamana na kushirikiana katika mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwania ya kuushinda ugonjwa wa UVIKO -19 ambao ni tisho kwa uhai na ustawi wa binadamu.
Kwa upande wake Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Ruvuma Rajabu Songambele amewashauri watoa huduma za Afya kuwafikia wananchi katika nyumba za ibada na makongamano mbali mbali ya kidini yanayofanyika katika jamii.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea DC.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.