Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewaomba viongozi wa Dini kuombea nchi ya Tanzania amani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28,2020.
Mndeme ameyasema hayo wakati anazungumza katika maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa kanisa la Menonite mjini Songea mkoani Ruvuma.Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amechangia ujenzi wa kanisa hilo tani tano za saruji zenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu.
“Endeleeni kuiombea nchi yetu tunasali hapa kwa sababu kuna amani wengine wanakimbia na masanduku na watoto kwasababu hakuna amani katika nchi zao”,alisisitiza Mndeme.
Mndeme amewaomba wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na watanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli pamoja na wasaidizi wake ili nchi ya Tanzania ipate maendeleo zaidi katika sekta mbalimbali.
Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Moroviani Usharika wa Songea mjini Selemani Nzyemba akizungumza kwa niaba ya Mchungaji wa Kanisa la Menonite amemshukuru Mkuu wa Mkoa na timu yake kwa kwa msaada wa vifaa vya ujenzi.
Amesema msaada huo ni mkubwa kwa kanisa hilo ambao utasaidia kuendeleza ujenzi na kwamba pia amemshukuru kwa kuacha majukumu yake na kufika kushiriki katika ibada ya kuazimisha mwaka mmoja tangu kuanzisha kanisa hilo mjini Songea.
Imeandaliwa na Farida Musa,Aneth Ndonde
Kutoka ofisi ya Habari ya Mkoa wa Ruvuma
Oktoba 12,2020.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.