MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amefanya mazungumza na madereva wa magari makubwa yanayobeba makaa ya mawe katika bandari ya nchikavu ya Kitai Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.Moja ya mambo ambayo Mndeme amesisitiza kwa madereva hao ni kutomwaga makaa ya mawe katika barabara ili kutoathiri mazingira na kuacha kuchanganya vyakula na makaa ya mawe kwa kuwa madini hayo ni sumu na hayatakiwa kuchanganywa na vyakula.Pia Mkuu wa Mkoa amewatahadharisha madereva kuchukuwa tahadhari wanapovuka kwenye madaraja na vivuko katika kipindi hiki cha mvua nyingi zinazoendelea katika Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma.SOMA HABARI KWA KINA HAPA https://www.youtube.com/watch?v=DdjT_hhlzoY
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.