Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas Novemba 7,2023 anatarajia kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2022 na Jan uari hadi Juni 2023.
Kanali Thomas atatoa taarifa hiyo Mubashara kupitia Luninga ya Channel Ten,moja kwa moja kutoka kwenye ukumbi wa Parokia ya Bombambili mjini Songea.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma katika taarifa hiyo atawasilisha mafanikio ya serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Ruvuma kwa kipindi cha miaka miwili na miezi 11 ya uongozi wake.
Taarifa hiyo itawasilishwa kwa wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Ruvuma,wadau mbalimbali wa maendeleo na wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.