Mkuu wa Wilaya Mbinga Mheshimiwa Aziza Mangosongo alifanya ziara ya kukagua mradi wa maji, shule ya watoto wenye mahitaji maalamu pamoja na kutembelea chama cha msingi cha ushirika cha Kigoti kilichopo kata ya maguu, Halmashauri ya Wilaya ya mbinga.
"Niwapongeze waliotoa maeneo ili kuruhusu uwekezaji huu ufanyike ili wananchi waweze kupata huduma ya maji na watoto wenye mahitaji maalamu waweze kusoma katika mazingira rafiki na karibu zaidi, Hivyo basi ni wajibu wetu wazazi kuhakikisha wanapata elimu badala ya kuwaficha nyumbani kusudi"
Sambamba na hilo alipokea taarifa kutoka kwa Meneja Ruwasa wilaya ya Mbinga na Mtendaji wa kata ya Maguu kuhusu miradi hiyo, Ambapo mradi wa maji utagharimu zaidi ya tshs milioni 700 na utahudumia zaidi ya watu elfu 16 na unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi na moja mwaka huu.
Alikadhalika mradi wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalamu umegharimu kiasi cha zaidi tshs milioni 200 ambapo fedha hizo zimetumika kujenga bweni moja na majengo 2 ya madarasa na matundu ya vyoo.
Aidha, baada ya kupokea taarifa na kufanya ukaguzi wa kina wa miradi hiyo Mhe. Mangosongo aliagiza dosari na changamoto zote zilizopo zifanyiwe marekebisho ili miradi ikamilike kwa wakati na iendane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na serikali.
Vilevile, Aliwataka kupima maeneo yote ya miradi ili kuepuka migogoro pindi ikikamilika, Pia alimtaka Meneja Tanesco wilaya kupeleka huduma ya umeme shuleni, sambamba na hilo aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu shughuli za maendeleo na kutoa taarifa za kuibiwa kwa vifaa wakati wa utekelezaji.
Mwisho, Alitembelea kigoti AMCOS ambapo aliwataka kuhamasisha wananchi kusajili ili waweze kupata pembejeo za kilimo, Vilevile aliwataka kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa sambamba na kuongeza wanachama pamoja na kuepuka migogoro isiyo na tija.
Sambamba na hilo alipokea taarifa kutoka kwa Meneja Ruwasa wilaya ya Mbinga na Mtendaji wa kata ya Maguu kuhusu miradi hiyo, Ambapo mradi wa maji utagharimu zaidi ya tshs milioni 700 na utahudumia zaidi ya watu elfu 16 na unatarajiwa kukamilika mwezi wa kumi na moja mwaka huu.
Alikadhalika mradi wa shule ya msingi ya watoto wenye mahitaji maalamu umegharimu kiasi cha zaidi tshs milioni 200 ambapo fedha hizo zimetumika kujenga bweni moja na majengo 2 ya madarasa na matundu ya vyoo.
Aidha, baada ya kupokea taarifa na kufanya ukaguzi wa kina wa miradi hiyo Mhe. Mangosongo aliagiza dosari na changamoto zote zilizopo zifanyiwe marekebisho ili miradi ikamilike kwa wakati na iendane na thamani halisi ya fedha zinazotolewa na serikali.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.