Ni muhimu sana tuwe tunafuatilia taarifa, wakati ATCL yetu (shirika linalofufuliwa) likitajwa kupata hasara ya shilingi Bilioni 60 kwa mwaka mmoja, na baadhi ya watu kuifanya kuwa ajenda kubwa na jambo la kushangaza sana, nataka mfuatilie pia hasara za baadhi ya mashirika makongwe na makubwa zaidi barani Afrika.
Mathalani, Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) limepata hasara ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 700 (mara 11 ya hasara ya ATCL) katika kipindi hicho hicho ambacho ATCL imepata hasara ya tzs Bilioni 60.
Na shirika la ndege kongwe zaidi Afrika, Ethiopian Airlines, limepata hasara ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Tzs Trilioni 1.1 (Bilioni 1,100) ambayo ni hasara kubwa mara 18.3 zaidi kuliko ATCL.
Sote hatufurahii hasara hata kama sisi tuna hasara ya Bilioni 60, lakini kwa sababu mbili tu za sasa... uchanga wa ATCL na dunia kuzongwa na KORONA zinaweza kuifanya ATCL ijikongoje, wakati mashirika makubwa kama KE Airlines na ETH Airlines yakizongwa pia na korona.
Pia kwa mwaka jana peke yake, mashirika makubwa zaidi ya ndege duniani, kama – Delta Air Lines, American Airlines, Lufthansa Group, United Airlines, Air France-KLM, na IAG yamerekodi hasara kubwa kabisa kihistoria ya zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 110 ambayo ni zaidi ya shilingi trilioni 2,500 za Tanzania.
Mwisho wa siku na katikati ya changamoto hizi, tunakubaliana kuwa ATCL inahitaji mikakati na mbinu za hali ya juu kibiashara ili itoke hapo ilipo, ikiwemo kuacha kabisa kufanya kazi kwa mazoea.
Imeandikwa na Julius Mtatiro
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.