Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Mheshimiwa Ngolo Malenya amesema kuwa Mwenge wa Uhuru katika Wilaya hiyo umefungua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi kumi ya maendeleo yenye thamani ya sh. bilioni 2.5
Malenya ameitaja miongoni mwa miradi hiyo kuwa ni mradi wa ujenzi wa barabara za lami mjini Namtumbo ambao unagharimu Zaidi ya shilingi milioni 889,mradi ambao unahusisha ujenzi wa wa barabara kwa kiwango cha changarawe,lami nyepesi,kokoto na uwekaji taa za barabarani 43.
Mradi mwingine ambao umepitiwa na Mwenge wa Uhuru ni ujenzi wa mabweni katika chuo cha Ufundi Stadi VETA Namtumbo,mradi ambao unatarajia kugharimu Zaidi ya shilingi milioni 814.
Mwenge wa Uhuru pia umepitia miradi ya lishe na shamba la miti katika Kijiji cha Luegu ambapo hadi kufikia mwaka 2023 shamba hilo lilikuwa na miti 5480 aina ya mitiki na kwamba mradi huo umegharimu shilingi milioni 45.
Mwenge wa Uhuru pia umepitia mradi wa chemchem ya maji ya asili iliyoboreshwa katika Kijiji cha Ruvuma Kata ya Hanga ambapo Zaidi ya shilingi milioni mbili zimetumika kuboresha chemchem hiyo.
Miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru wilayani Namtumbo ni kituo cha mafuta cha KSM kilichoanzishwa na Said Kazibure ambapo hadi sasa mradi umegharimu shilingi milioni 515 na kwamba mradi unatarajia kutoa ajira 25.
Mwenge wa Uhuru umepokea taarifa ya ugawaji wa vyandarua kwa akinamama wajawazito,makundi maalum na Watoto chini ya mwaka mmoja,pia Mwenge wa uhuru umepokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za ukatili wa kijinsia na watu wenye ulemavu.
Akizungumza baada ya kukagua mradi wa barabara za lami mjini Namtumbo,Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godref Mnzava ameipongeza TARURA kwa usimamizi mzuri wa mradi huo ambao pia umezingatia mfumo wa ununuzi wa umma katika utekelezaji wake.
Amesema serikali inaendelea kuelekeza manunuzi yote na zabuni zake yapite kwenye mfumo wa manunuzi wa kidigitali wa NEST ambapo amewapongeza TARURA kwa kutekeleza agizo hilo kwa kupitisha zabuni kwenye mfumo hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.