Mwenge wa Uhuru 2024 umetembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara za lami nzito zinazogharimu Zaidi ya shilingi bilioni 22 katika mji wa Songea mkoani Ruvuma.
Akitoa taarifa ya mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru,Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Wakili Bashir Muhoja amesema Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 12 zilizobahatika kupata mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara za lami nzito zenye urefu wa kilometa 10.1.
Amebainisha mradi huo una jumla ya barabara 20 za lami katikati ya Mji wa Songea ambazo zitatengezwa kupitia mradi huo ambao umefadhiliwa na Jumjuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) kupitia Benki ya Dunia kwa ajili ya kuboresha miundombinu na ushindani wa miji,Manispaa na Majiji nchini Tanzania (TACTC).
Hata hivyo amebainisha kuwa mradi huo unaratibiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI na kwamba hadi sasa Mkandarasi amefikia asilimia 20 ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara hiyo.
“Ujenzi wa barabara hizi utaleeta manufaa ya kuwa na miundombinu bora na inayopitika wakati wote
hivyo kuwezesha watumiaji wa barabara kupunguza gharama za uendeshaji wa vifaa vya moto,kutoa ajira kwa wananchi 134 na kuimarisha ulinzi na usalama kwa kuwa barabara hizo zitakuwa na taa’’,alisisitiza.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava ameagiza Mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili uanze kuwahudumia wananchi wa Mji wa Songea.
Mwenge wa Uhuru pia umeweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea ambao unatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 500.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava pia amekubali kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa vyumba kumi na matundu kumi katika shule ya sekondari ta Londoni Manispaa ya Songea,mradi ambao unagharimu Zaidi ya shilingi milioni 259.
Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Manispaa ya Songea umetembelea mradi wa maji Mtaa wa Pambazuko Kata ya Tanga unaogharimu Zaidi ya shilingi milioni 578 wenye uwezo wa kuhudumia wananchi wapata0 15,990.
Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Ustawi wa Mazingira Songea (SOUWASA) kwa kushirikiana na Wizara ya Mazingira.
Mwenge wa Uhuru pia umepitia taarifa ya mapambano dhidi ya malaria kwa ugawaji wa vyandarua kwa mama wajawazito,makundi maalum na Watoto chini ya mwaka mmoja ambapo hadi sasa vyandarua vyenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 356 vimegawiwa bure.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.