KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi katika mradi wa maji uliopo katika Kijiji cha Tuwemacho Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma mradi ambao unatekelezwa kwa kiasi cha sh. Bilioni 1,054,232,603.55 na mpaka sasa kiasi cha sh. 138,134,890.00 zimetumika kumlipa mkandarasi.
Mradi huo ambao unatekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) umesanifiwa kuhudumia wananchi wapatao 3527 katika Kijiji cha Tuwemacho.
Awali akiweka jiwe la msingi mradi huo kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava alisema kuwa ameridhishwa na mradi huo baada ya kukagua miundombinu, Nyaraka na kuangalia usimamizi ulikuwaje hivyo Mwenge wa Uhuru umejiridhisha na usimamizi wote uliofanyika kwenye mradi huo pasipo na shaka yoyote.
" Nitoe angalizo kwa wananchi ambao tunapata huduma hii muhimu ya maji, tuwe makini kutunza miundombinu hii, tuwe makini kutunza vyanzo vya maji na mabomba ambayo yanatupatia huduma hii muhimu sisi sote tunajuwa kwamba maji ni huduma muhimu sana na uwepo wa maji unaleta faraja kubwa sana kama tunavyoona akina mama wanashangilia kwa kuwa mradi huu umetakuwa na manufaa makubwa" alisema Mnzava.
Akisoma taarifa Taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Injinia Maua Mgallah alisema kuwa mradi huo wa maji ulianza January 5/2024 na kutarajiwa kukamilika Julai 4 mwaka huu.
Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la ukosefu wa huduma ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.