Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma imefanya kikao kazi kilichowajumuisha Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Awali na Msingi kwa lengo la kufanya tathmini ya mwenendo wa elimu, kuwajengea uwezo viongozi wa shule, na kuweka mikakati ya kuinua kiwango cha elimu kwa mwaka 2025.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Nyasa, Bw. Pasifiki Mhapa, amewataka walimu kuwa wabunifu na kuwasaidia wanafunzi ili kuboresha ufaulu wilayani humo. Aidha, amesisitiza kuwa walimu wanapaswa kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii kwa kuwalea na kuwafundisha wanafunzi ili waweze kufaulu na kuleta maendeleo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.