OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma imepokea mipira 1000 iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia program ya Football For Schools kwa ajili ya kuendeleza michezo katika shule za msingi na sekondari.
TFF imetoa mipira hiyo ikiwa ni jitihada za Rais wa Shirikisho hilo kumuunga mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo nchini Tanzania.
Akizungumza kwenye hafla hiyo kabla ya kukabidhi vifaa hivyo,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amewashukuru TFF na kumpongeza Rais Samia kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kukuza sekta ya michezo.
“Rais Samia ana maono makubwa ya kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika michezo ya ndani na nje ya mipaka ya nchi’’,alisisitiza.
Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma umekuwa na maendeleo ya wastani katika michezo ambapo ameupongeza uongozi wa Chama Cha Mpira wa Miguu mkoani Ruvuma FARU kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maendeleo ya soka kwa wanawake.
Katika hafla hiyo jumla ya mipira 800 kati ya 1000 iligawiwa katika shule za msingi na sekondari zilizopo katika Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma,
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.