MAAFISA wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma wamepongezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) kwa kuwataarifa wananchi kwa kusahihi mafunzo ya utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yaliofanyika kwa siku tano katika hoteli ya Tiffany Diamond mjini Mtwara.
Akizungumza wakati wa ufungaji mafunzo hayo ambayo yalishirikisha timu za dharura za kukabili magonjwa kutoka mikoa hatarishi ya Ruvuma na Mtwara,Valentina Sanga wa Idara ya Maafa Dawati la Afya Moja Ofisi ya Waziri Mkuu,amesema wanahabari hao licha ya kushiriki katika mafunzo hayo pia wamekuwa wanatimiza kazi ya kuhabarisha umma kwa siku zote za mafunzo kupitia vyombo mbalimbali vya habari
Ametoa rai kwa wanahabari wengine nchini kuiga mfano wa wanahabari hao ambao pia katika mafunzo hayo katika mtihani wa mwisho wa kujipima wamefanya vizuri na kupewa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo.
Sanga amelishukuru Shirika la FAO kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kufanikisha mafunzo hayo na kuwapongeza wakufunzi wote kutoka Chuo cha SUA,Wizara ya Afya na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kufanikisha mafunzo hayo ambayo yamesaidia kuelewa dhana ya afya moja ambayo itasaidia kupunguza gharama kwa kushirikiana.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani Dr.Niwael Mtui amesema wanahabari hao wamefanya kazi iliyotukuka na kwamba wanastahili pongezi kwa sababu wamekuwa wanapigiwa simu kutoka sehemu mbalimbali kutokana na kusoma na kuangalia habari mbalimbali zilizochapishwa kwenye magazeti,redioni,luninga za mitandaoni na kutangazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kihabari.
“Wanahabari ni miongoni mwa wadau wanaounda timu za dharura za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko,wadau wengine ni wataalam wa afya,mifugo,mazingira,maliasili hivyo naomba mafunzo yote ambayo tumepata twende kushare na wenzetu ambao hawajapata nafasi ya mafunzo’’,alisema.
Dr.Mtui amesisitiza kuendelea kushirikiana na kwamba ndani ya siku tano wadau wameweza kufahamiana jambo ambalo litakuwa rahisi kushirikiana kwa kupeana taarifa za milipuko ya magonjwa sita ya kipaumbele Ili kuchukua hatua haraka.
Naye Mwakilishi wa washiriki wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Jairy Khanga ameipongeza Ofisi na Waziri Mkuu na FAO kwa kutoa mafunzo ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara.
“Hii ndiyo mikoa pekee ambayo ilikuwa haijapata mafunzo hayo,mikoa hii ya kusini ambayo inapakana na nchi jirani ipo katika hatari ya kupata magonjwa ambukizi ya mlipuko hivyo mafunzo haya ni muhimu sana’’,a asisitiza Dr.Khanga.
Imeandikwa na maafisa Habari serikalini
Oktoba 20,2020
Mtwara
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.